Dkt. Saeed Abdulrahman Abu Ali...Kiongozi wa Sheria na Siasa wa Kipalestina katika Msingi wa Ushirikiano wa Kiarabu
Imetafsiriwa na: Nermeen Khaled
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Kutoka Jenin hadi ukumbi wa Chuo cha Nchi za Kiarabu, na kutoka kumbi za mihadhara hadi korido za maamuzi ya kisiasa, Profesa Dkt. Saeed Abdulrahman Abu Ali amechora safari ya kipekee iliyounganisha kazi ya kitaaluma, kisiasa, na kidiplomasia, na kumfanya kuwa mmoja wa sura mashuhuri za kisheria na kisiasa nchini Palestina na katika eneo la Kiarabu.
Dkt. Saeed amezaliwa mwaka 1955 katika mji wa Jenin, na alianza safari yake ya kielimu katika vyuo vikuu vya Tunisia na Ufaransa, akipata shahada kadhaa mashuhuri, zikiwemo:
• Shahada ya Udaktari ya Taifa katika Sayansi ya Kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Tunisia mnamo mwaka 1995
• Shahada ya Udaktari katika Masuala ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Toulouse, Ufaransa, mnamo mwaka 1992
• Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Kisiasa
• Diploma katika Usimamizi wa Taasisi za Serikali kutoka Chuo Kikuu cha Harvard
Maisha ya kitaaluma hayakuwa sehemu pekee ya safari yake; Dkt. Saeed ameshikilia nyadhifa nyingi za uongozi ndani ya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina, ikiwemo kuwa Gavana wa Nablus, kisha Ramallah na Al-Bireh, na baadaye Waziri wa Mambo ya Ndani kati ya mwaka 2009 na 2014. Aidha, alifanya kazi kama mshauri wa kidiplomasia nchini Tunisia na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na Habari katika ofisi ya Rais.
Tangu mwaka 2015, Dkt. Saeed amekuwa Katibu Mkuu Msaidizi, Mkuu wa Sekta ya Palestina na Ardhi Zilizokaliwa za Kiarabu katika Chuo cha Nchi za Kiarabu, akiongoza juhudi kubwa katika kutetea suala la Palestina na kupinga miradi ya ukoloni wa walowezi na uislamishaji, hususan katika mji wa Yerusalemu.
Kitaaluma, Dkt. Saeed anaendelea na safari yake kama Profesa wa Sheria ya Umma na Sayansi ya Kisiasa katika vyuo vikuu kadhaa vya Kipalestina, na pia amesimamia tasnifu nyingi za kielimu na alikuwa mhakiki wa kielimu aliyeidhinishwa katika wizara za Elimu ya Juu na Sheria nchini Palestina. Aidha, ameshiriki katika mikutano mingi ya kielimu ya kikanda na kimataifa, na ana machapisho ya kitaaluma, miongoni mwao kitabu kuhusu Mahakama ya Kikatiba ya Palestina na kingine kuhusu hali ya mji wa Yerusalemu. Pia amechangia katika kuhariri majarida maalumu kama vile "Palestina – Mwezi", "Shu’un Arabiya", na "Al-Maqdisiyya".
Katika utu wake unadhihirika sura ya kiongozi wa taifa, mtafiti, msomi, na mwanaharakati wa Kiarabu, ameyeweka maisha yake kwa ajili ya Palestina na masuala ya umma wa Kiarabu.