Sharif Gad… Daraja la Kitamaduni kati ya Kairo na Moscow, na Sauti ya Kiarabu katika vikao vya kimataifa

Sharif Gad… Daraja la Kitamaduni kati ya Kairo na Moscow, na Sauti ya Kiarabu katika vikao vya kimataifa

Imetafsiriwa na: Nourhan Reda
Imehaririwa na: Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Kutoka Moscow hadi Kairo, na kutoka sherehe za vijana hadi vikao rasmi vya kitamaduni, Sharif Gad ameunda safari ya kipekee iliyomfanya kuwa moja ya alama kuu za ubadilishanaji wa kitamaduni kati ya dunia ya Kiarabu na Urusi, na kuwa kiongozi mashuhuri katika uwanja wa habari na kazi za kimataifa za kitamaduni.

Safari yake ilianza mjini mkuu wa Urusi, ambapo alihitimu katika Kitivo cha Habari cha Chuo Kikuu cha Moscow mnamo mwaka 1986, kisha akaendelea kukuza ustadi wake wa kisanii kwa kupata kozi ya uongozaji na upigaji wa sinema katika Taasisi maarufu ya Filamu ya Moscow mnamo mwaka 1987, jambo lililoonekana baadaye katika uwepo wake wa vyombo vya habari na ubunifu katika anga la Kiarabu.

Kati ya mwaka 1988 na 1991, alifanya kazi kama mhariri wa habari katika magazeti "Al-Ahali" na "Sawt Al-Arab", akiwaletea wasomaji masuala ya kitamaduni na jamii kwa mtazamo halisi, wa akili, wenye busara, wazi na wa kisasa, kabla ya kuhamia kazi ya kitamaduni ya taasisi, ambapo aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Kiarabu wa Kituo cha Utamaduni cha Soviet mnamo mwaka 1988.

Tangu mwaka 1991 hadi leo, Sharif Gad anaendelea kuongoza shughuli za kitamaduni katika Kituo cha Utamaduni cha Urusi mjini Kairo, akichangia kuimarisha mazungumzo ya kitamaduni kati ya mataifa, na kuanzisha majukwaa ya maarifa yaliyoziunganisha vizazi mbalimbali pamoja na uzoefu wa kielimu na kitamaduni wa Urusi.

Ameanzisha Jumuiya ya Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Urusi na Soviet nchini Misri, iliyokuwa kama nyumba ya pamoja kwa wote waliowahi kusoma huko, na pia aliongoza Umoja wa Kiarabu wa Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Urusi na Soviet kwa vipindi viwili: 2004-2006 na 2018-2022, akithibitisha uwepo wake kama kiongozi wa kikanda katika muktadha huo.

Majukumu yake hayakuishia kwenye jumuiya hizo tu, bali pia ni Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Filamu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Urafiki wa Misri na Urusi, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika wa Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Urusi na Soviet, nyadhifa hizi zikionyesha ushiriki wake wa kina katika uwanja wa kitamaduni na kikanda.
Sharif Gad alikuwa kiongozi wa ujumbe wa Misri kwenye Tamasha la Vijana Ulimwenguni lililofanyika mjini Sochi, Urusi mwaka 2017, na pia aliongoza Mkutano wa Kiarabu wa Wahitimu wa Vyuo Vikuu vya Urusi na Soviet uliofanyika Kairo mnamo Novemba 2018, ukiwahusisha nchi 14 za Kiarabu. Katika toleo la tamasha hilo la mwaka 2024, alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Ujumbe wa Misri tena huko Sochi, akithibitisha hadhi yake inayotambulika katika vikao vya kimataifa.

Sharif Gad bado ni mfano wa mchangamfu wa kitamaduni, mhitimu ambaye hakusahau mizizi yake ya kitaaluma, bali ameigeuza kuwa mradi kamili wa mawasiliano ya kibinadamu na ushirikiano kati ya mataifa.