Mohamed Al-Kousi: Safari ya Kipekee ya Habari katika Huduma ya Umoja wa Mataifa na Maendeleo Endelevu
Imetafsiriwa na: Mohamed Mahmoud Badawy
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Katika kipindi ambacho dunia inashuhudia mabadiliko ya kasi na changamoto zinazoongezeka katika sekta ya vyombo vya habari na mahusiano ya kimataifa, jina la Mohamed El-Kousi limeibuka kama miongoni mwa majina mashuhuri ya Kiarabu katika nyanja za mawasiliano ya kimkakati na uanahabari wa maendeleo.
Kwa sasa, El-Kousi anahudumu kama Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa Misri na Saudi Arabia, akiendesha juhudi za mawasiliano zinazolenga kuimarisha malengo ya Umoja wa Mataifa na kusimulia simulizi za maendeleo endelevu, hususan katika muktadha wa Misri.
El-Kousi ana zaidi ya miaka 20 ya uzoefu katika mawasiliano jumuishi, mahusiano ya kimkakati ya vyombo vya habari, na ujenzi wa ushirikiano na wadau kutoka sekta za umma na binafsi. Amewahi kushikilia nyadhifa za juu katika taasisi mashuhuri, zikiwemo:
• Mkurugenzi Mkuu wa Active PR, mshirika wa Kimasri wa kampuni ya kimataifa Burson-Marsteller.
• Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara katika Tetra Pak Misri, mojawapo ya kampuni kubwa zaidi duniani katika sekta ya ufungashaji wa vyakula.
• Mkurugenzi wa Kikanda wa Masoko katika British Airways kwa Misri na Afrika Kaskazini, ambapo alisimamia kampeni zilizofanikiwa katika soko lenye ushindani mkubwa.
Safari ya kazi ya El-Kousi inatambulika kwa uwezo wake wa kubuni kampeni zenye ushawishi, kuongoza timu za tamaduni mbalimbali, na kujenga mazungumzo ya kujenga na jamii husika. Sifa hizi zimemfanya kuaminiwa na mashirika ya kimataifa na ya ndani.
Katika ushiriki wake ujao kwenye moja ya mijadala, El-Kousi alibainisha azma yake ya kutumia dakika 15–20 kwa hotuba, kisha kufungua mjadala kwa maswali kutoka kwa hadhira kwa takribani saa moja. Hii inadhihirisha mtindo wake wa mawasiliano unaosisitiza kusikiliza kwa makini na kubadilishana mawazo kwa dhati.
Uzoefu wake unawakilisha mfano bora wa muunganiko kati ya utaalamu wa mawasiliano na kazi ya maendeleo ya kimataifa, ukithibitisha nafasi muhimu ya vyombo vya habari katika kuendeleza maendeleo na kudumisha amani, katika ngazi za kikanda na kimataifa.