Kwa Ufadhili wa Rais wa Jamhuri ... waombaji 774 kwa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika 

Kwa Ufadhili wa Rais wa Jamhuri ... waombaji 774 kwa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika 

Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kupokea maombi 774 ya kujiunga na kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaofanyika kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, chini ya kauli mbinu "Ushirikiano wa Kusini - Kusini", na ulipangwa kufanyika mjini Kairo mnamo nusu ya kwanza ya Juni ijayo.

Ambapo takwimu ya waliojiandikisha kushiriki katika kundi la pili la "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" ilifikia watu 774 wa jinsia mbili, ambapo kiasi cha wanaume kilikuwa karibu 63.8%, wakati kiasi cha wanawake kilikuwa karibu 36.2%. na wastani wa umri wao uko katika kundi la umri kutoka miaka 25 hadi 34 ulifikia karibu 46.3% ya kati yao, 62.7% ni wanawake, 37.3% ni wanaume kwa ujumla, na kundi la umri kutoka miaka 20 hadi 24, kwa kiwango karibu  33.5% kati yao wanawake 61% na wanaume 39% huku kiasi cha  walio na umri kuanzia miaka 35 hadi 40 ni takribani 20.2% ya waombaji wote ni 67.5% tu wanawake na 32.5% wanaume.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Misri baada ya Urais wake kwa Umoja wa Afrika mnamo wa 2019 katika kutekeleza jukumu lake husika kuimarisha jukumu la vijana waafrika kwa kutoa aina zote za msaada, uwezeshaji na kutoa mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika cheo cha uongozi na kufaidika na uwezo na mawazo yao.  

 Pia unachukuliwa kama mojawapo ya mbinu za kutekeleza yote Kutoka (Mtazamo wa Misri 2030 - Misingi Kumi ya Shirika la Mshikamano wa Afro-Asia - Ajenda ya Afrika 2063 - Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 - Ushirikiano wa Kusini-Kusini- Mwongozo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji kwa Vijana - Hati ya Vijana wa Afrika).

Udhamini huo unalenga viongozi 100 wa vijana katika (Afrika - Asia - Amerika ya Kusini) wakiwakilisha 50% wanaume 50% wanawake kutoka kwa walengwa wa watoaji wa maamuzi katika sekta ya umma, wahitimu wa programu ya Wajitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi wakuu katika sekta binafsi, wanaharakati wa jamii ya kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa kwa vijana, wajumbe wa mabaraza ya mitaa, viongozi vijana wa vyama, Wanachuoni wa Vyuo Vikuu, watafiti katika vituo vya Tafiti za kimkakati na mawazo, wanachama wa mashirika ya kitaaluma, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, wajasiriamali wa kijamii, na nyanja nyingine nyingi.

Ikumbukwe kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi ulitekelezwa mnamo Juni 2019, pamoja na Ufadhili wa Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly, uliolenga viongozi vijana wenye taaluma mbalimbali za utendaji ndani ya jamii zao ili kuwasilisha Jaribio la Maendeleo la Misri katika uimarishaji wa taasisi na kuandaa kwa Uhusika wa kitaifa.