Wanafunzi wa Udhamini wa Nasser wako kwenye Klabu ya Sinema ya Kiafrika
Miongoni mwa shughuli za siku ya tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, unaotolewa kwa Wizara (Ofisi ya vijana waafrika na idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuli "Waziri Mkuu", mnamo kipindi cha tarehe ya 8 hadi 22 Juni, 2019,kwa ushirikiano wa Shirikisho la vijana waafrika..
Vijana walioshiriki walitembelea Sinema ya El Hanager, ambapo filamu mbili zilioneshwa, "Simbeen" na "Photocopy", na sherehe iliyotolewa na msanii, Mohamed Galal, Mkurugenzi wa ofisi ya tamasha la Luxor la filamu la Afrika ilianza kwa maneno kuhusu Sinema ya Kiafrika na shughuli za klabu, kisha mchambuzi wa kisanaa Farouk Abdel Khaleq, Mkuu wa Shirika la Wasanii Vijana, alitoa hotuba aliwakaribisha Vijana waafrika.
Alieleza furaha yake kubwa kwa kusherehekea Mtoaji Sinema wa Senegal Othman Sembine katika kumbukumbu yake, kisha Mwandishi wa Script Ahmed Helba, Mratibu mkuu wa Tamasha hilo, alizungumzia shughuli za klabu, na umuhimu wake katika kutoa filamu za Kiafrika zilizoshinda tuzo kutoka kwa Tamasha la Luxor, na upanuzi wa shughuli zake kwa Mikoa mbalimbali ya Misri. Pia, Mwigizaji Yasmine El Hawary alizungumza kwa Niaba ya M Azza El Husseini, Mkurugenzi wa Tamasha, kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya Mtoaji Sinema Marehemu wa Senegal Othman Sembine maadhimisho hayo yanayofanyika katika nchi 38 za Afrika kwa wakati mmoja kupitia mradi wa "Sembene Across Africa".
Pia, Hassan Ghazaly , Makamu wa Rais wa Umoja wa Vijana wa Afrika, alizungumza na kutoa hotuba kuhusu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, na kabla ya Kuonesha Filamu hizo mbili Mwandishi wa muswada Sayed Fouad, Mkuu wa Tamasha la Luxor African Film, linaloandaliwa na klabu hiyo kwa Ushirikiano na Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni unaoongozwa na Dokta Fathi Abdel Wahab, alihitimisha kauli mbapo aliwakaribisha Vijana waafrika nchini Misri wakati wa Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, pia alizungumzia Tamasha la Filamu za Kiafrika na nafasi yake katika kutambua Tamaduni za Kiafrika na mchango wa Sinema wa kuwaunganisha watu pamoja.
Katika hafla ya kumbukumbu ya Marehemu mwongozaji Sinema wa Senegal Othmane Sembene, akijulikana kama Mwanzilishi wa Sinema ya Kiafrika, Filamu ya "Sembene" ya wawongozaji wa Sinema wawili Samba Gadjego na Jason Silverman ilionyeshwa. Filamu hiyo inahusu maisha ya Sembene, aliyezaliwa mwaka 1923 na kuaga Dunia 2007.
Kisha filamu ya Misri "Photocopy" iliyotolewa na Tamer Ashry na kuandikwa na Haitham Dabour na kuigiza na Mahmoud Hemida, Sherine Reda, Farah Youssef, Bayoumi Fouad, Ali Al-Tayeb, Youssef Othman na Ahmed Dash, iliyoandikwa na Haitham Dabour, iliyotolewa na Tamer Ashry. , na kutayarishwa na "Red Star". Filamu hiyo inamhusu Mahmoud, Mwanamume akiwa kwenye mwisho wa miaka hamsini ambaye anamiliki maktaba ya Photocopy kwenye mtaa wa Abdo Pasha. Anapoombwa kuchapisha karatasi za utafiti kuhusu kutoweka kwa Dinosau, Suala hilo linamtia wasiwasi. Anahisi kwamba hiyo itaeleza kuzorotesha hali yake ya kifedha na idadi ya wateja wake, inayopungua siku baada ya siku.