Mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana , ni raisi wa umoja wa Wanafunzi wa Afrika nchini Misri
Jana, Jumatano, katika Jumuiya ya Afrika, mwanachama wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, Abd El Rahman Sayed Al-Mukhtar, alitawazwa kama Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi waafrika nchini Misri, ikiwa ni miongoni mwa uchaguzi wa kila mwaka wa ofisi ya kiutendaji wa Umoja mkuu.
Abd El-Rahman Sayed Al-Mukhtar pia amewahi kuwa mratibu wa kitaifa wa Evidence-based Medicine, Na ni kocha wa kimataifa wa elimu ya matibabu na Shirikisho la Kimataifa la Wanafunzi wa Matibabu - Misri na kama katibu mkuu, na katibu wa kiutamaduni na kitaaluma wa Umoja Mkuu wa Wanafunzi waafrika nchini Misri pia.
Pia alichaguliwa akiwakilisha Mauritania kwa shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Chain. Pia anachukuliwa kuwa mmoja wa viongozi vijana waafrika nchini Mauritania, katika nyanja za kazi za kijamii na matibabu, na alikuwa mgeni katika mahojiano mengi na mazungumzo ya vijana huko Misri na Mauritania.
Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu kutoka Mauritania kuongoza Umoja mkuu wa Wanafunzi waafrika nchini Misri ulioanzishwa mnamo 1986 mjini Kairo ukiwa na Ufadhili wa Jumuiya ya Afrika.