Abd El Moneim Riad
Luteni Jenerali Abd El Moneim Riad alizaliwa katika kijiji cha seberbay, moja ya vitongoji vya Tanta, Mkoa wa Gharbia, Oktoba 22 , 1919. Familia yake ilihamishwa kutoka Fayoum. Baba yake alikuwa mwenye nafasi ya (Kanali sasa), Muhamed Riyad Abdullah kamanda wa vitalu vya wanafunzi Kitivo cha Vita. ambapo viongozi wengi wa Shirika la kijeshi walipata mafunzo Pamoja naye.
Anazingatiwa mmoja wa wanajeshi waarabu mashuhuri katika nusu ya pili ya karne ya ishirini, ambapo alishiriki katika Vita vya Dunia vya pili dhidi ya Wajerumani na Waitaliano kati ya 1941 na 1942, na akashiriki katika vita vya Palestina mnamo 1948, uchokozi wa nchi tatu mnamo 1956, vita ya 1967 na vita ya kudhoofisha, pia alisimamia mpango wa kimisri wa kuharibu mstari wa Berlif wakati wa vita ya kudhoofisha.
Elimu yake:
Alisoma katika Masomo ya kijijini na akamaliza masomo hadi alipata shule ya upili kutoka Shule ya Khedive Ismail.
Akamaliza masomo yake katika kitivo cha Jeshi mnamo 1938 akiwa na nafasi ya Luteni wa pili.
Akapata shahada ya Uzamili katika Sayansi za kijeshi mnamo 1944 na akashika nafasi ya kwanza.
Akatimiza masomo yake kama mwalimu wa mizinga ya kulipulia ndege kwa Ubora huko Uingereza mnamo 1945 na 1946.
Akafahamu vizuri lugha kadhaa zikijumuisha Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani na Kirusi.
Pia alijiunga na Kitivo cha Sayansi kusoma hisabati safi.
Wakati alikuwa kama Jenerali, alijiunga na kitivo cha Biashara; akiwa na imani ya mkakati ni uchumi.
Akatimiza masomo yake katika Chuo cha Kijeshi cha Juu cha Naser, na akapata Urafiki wa kitivo cha Vita cha Juu mnamo 1966.
Maisha yake ya Kijeshi:
Mnamo 1941 aliteuliwa baada ya kuhitimu masomo katika silaha ya mizinga, na aliambatanishwa na betri moja dhidi ya ndege katika eneo la Magharibi, ambapo alishiriki katika vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Ujerumani na Italia.
Mnamo 1947-1948, alifanya kazi katika Idara ya Operesheni na Mipango huko Kairo. alikuwa kama mpatanishi na mratibu kati yake na uongozi huko Palestina, na alipewa Nishani ya ustahiki ya dhahabu kwa uwezo wake wa kijeshi ulioonekana wazi wakati huo.
Mnamo 1951, alichukua uongozi wa shule wa mzinga la kulipua ndege, na alikuwa yenye nafasi ya kanali.
Mnamo 1953 aliteuliwa kama kamanda wa Jenerali wa kwanza wa kupambana na ndege huko Aleskandaria.
Kuanzia Julai 1954 hadi Aprili 1958 alichukua agizo la ulinzi wa kulipua ndege katika silaha ya mzinga.
Mnamo Aprili 9, 1958, alisafiri katika misheni ya kielimu kwa Umoja wa Kisoviet ili kumaliza kozi ya kimkakati katika Chuo cha Juu cha Jeshi. _Alimaliza mnamo 1959 kwa ubora na aliitwa huko kama Jenerali wa Dhahabu.
Mnamo 1960, alirudi kama Mkuu wa Wafanyikazi wa Silaha ya Mizinga._
Mnamo 1961, Naibu Mkuu wa idara ya uendeshaji, akiongozwa na Wakuu wa Wafanyikazi wa Wanajeshi alipewa nafasi ya Mshauri wa uongozi wa Jeshi la Anga kwa masuala ya ulinzi wa anga.
Mnamo 1964 aliteuliwa Mkuu wa Wafanyikazi wa uongozi wa Umoja wa kiarabu.
Mnamo 1966 alithaminiwa akawa Jenerali.
Mnamo Mei 1967, na baada ya usafirishaji wa Mfalme Hussin kwenda Kairo; kusaini Mkataba wa Ulinzi wa Pamoja, Jenerali huyo aliteuliwa kama kamanda wa Kituo cha uongozi cha kuendeleza huko Oman.basi akafikia pale Juni mosi 1967 na baraza dogo la wafanyakazi la maafisa waarabu kuanzisha kituo cha uongozi.
Wakati vita vya 1967 vilipoanza, Jenerali aliteuliwa kama Kamanda Mkuu wa Medani ya Yordani.
Mnamo Juni 11, 1967, alichaguliwa kama Mkuu wa Wafanyikazi wa vita vya Vikosi vya Silaha vya Misri. pamoja na Waziri wa Vita na Kamanda mpya wa Mkuu wa Majeshi, Jenerali wa kwanza Mohamed Fawzi, walianza kuijenga tena na kuipanga.
Mnamo 1968, aliteuliwa kama Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuyia ya Nchi za kiarabu.
Jenerali alipata ushindi wa kijeshi katika vita vilivyopigwa na vikosi vya kijeshi vya Wamisri wakati wa vita vya kudhoofisha, kama vile Vita vya Ras al-Ush, ambamo jeshi dogo la askari la miguu likazuia udhibiti wa vikosi vya Israeli kwenye mji wa Misri wa Por Fouad iliyoko kwenye mfereji wa Suez, mwishoni mwa Juni 1967, na uharibifu wa mwangamizi wa Israel wa Eilat mnamo Oktoba 21, 1967 na kuangusha kwa baadhi ya ndege za kivita za Israeli mnamo miaka 1967 na 1968, na uharibifu wa 60% ya ngome ya mstari wa Barlif, uliogeuka kutoka kwa mstari wa kujitetea kwa onyo la mapema tu.
Nishani na Medali:
Medali ya huduma ndefu na mfano mzuri.
Nishani ya nyota wa Heshima.
Nishani ya Ustahiki ya Dhahabu.
Nishani ya kitaifa ya mwerezi na degree ya afisa mkubwa kutoka Lebanon.
Nishani ya Sayari ya Yordoni tabaka la kwanza.
Kifo chake:
Machi 8 asubuhi, Jenerali aliamua kuelekea binafsi yake kwa Medani kuangalia matokeo ya vita, na aliamua kutembelea eneo lenye maendeleo makubwa Zaidi. Halafu, ghafla moto wa vikosi vya Israel ullianza ndani ya eneo ambapo alikuwa Pamoja na maaskari wake, kifaru kimoja karibu na Shimo, na aliaga Dunia kutokana na Majeraha ya mabaki ya bomu.