Chuo cha Kijeshi cha Misri… Taa mpya ya kuwaandaa viongozi wa baadaye katikati ya mji mkuu wa kiutawala
Imetafsiriwa na: Shahd Mohamed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Katika hatua ya kimkakati inayoakisi dira ya serikali ya Misri ya kusasaisha mfumo wa mafunzo ya kijeshi, Chuo cha Kijeshi cha Misri kilianzishwa kama taasisi ya juu ya kuandaa viongozi wa baadaye wa vikosi vya jeshi, kwa mujibu wa Sheria Namba 149 ya mwaka 2022.
Chuo hiki kiko katika eneo la kipekee ndani ya Kituo cha Amri ya Kimkakati cha serikali katika Mji Mkuu wa Utawala Mpya, na kinasimamiwa na Waziri wa Ulinzi wa Misri, jambo linalokipa uzito wa kitaasisi na kuhakikisha viwango vya juu vya nidhamu na ubora wa elimu.
Lengo la chuo hiki ni kuhitimisha maafisa wa kitaalamu na kiufundi, wanaoweza kukidhi mahitaji ya huduma katika vitengo mbalimbali vya vikosi vya jeshi, iliokubaliana na changamoto za kijeshi na kiusalama za kisasa.
Maono haya yanatekelezwa kupitia muundo wa kitaaluma unaojumuisha vyuo vinne maalum, vinavyotoa shahada ya kwanza au leseni kulingana na mtaala, ndani ya mfumo wa ubora wa kisayansi na kijeshi.
Chuo cha Kijeshi cha Misri ni mfano halisi wa dhana ya serikali ya kisasa, inayochanganya uzoefu wa kivita na maarifa ya kitaaluma, ili kujenga vizazi vipya vya maafisa wanaoweza kuongoza kwa ujasiri na umahiri.