Dini kulingana na mawazo ya Gamal Abd El Nasser

Dini kulingana na mawazo ya Gamal Abd El Nasser
imeandikwa na Dokta Amr Sabeh
- Katika kitabu cha (Falsafa ya Mapinduzi ) cha Gamal Abd El Nasser kilichotolewa mnamo 1954, Abd El Nasser alijadili masuala matatu ambazo sera ya kimisri ya nje itaelekea ndani yake , pamoja na sehemu ya Kiislamu inayoingiliana na sehemu ya kiarabu na ya Kiafrika.
Khalifa mkubwa Abu Bakr Al-Siddiq ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza kukusanya Qur'ani Tukufu katika kitabu tukufu cha Mwenyezi Mungu , baada ya kusisitiza kutoka kwa Omar bin Al-Khattab,Ridha ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, baada ya mauaji ya wengi wa wanaohifadhi Qurani katika vita vya Uasi . Na Khalifa Mkubwa Othman Bin Afan ni mwenye kitabu tukufu cha kwanza kinachomo sura za Qurani tukufu. Na Rais Gamal Abd El Nasser ndiye mtawala mwislamu wa kwanza katika historia, ambapo wakati wa utawala wake Qur'ani Tukufu ilikusanyiwa ikisikiliziwa (iliyosomwa na ya sasa) katika mamilioni ya matepi na rekodi kwa sauti za wasomaji wamisri.
Wakati wa enzi ya Gamal Abd El Nasser, idadi ya misikiti nchini Misri iliongezeka kutoka misikiti elfu kumi na moja kabla ya mapinduzi kwenda elfu ishirini na moja mwaka 1970, ikimaanisha kuwa wakati wa utawala wa miaka 18 kwa Rais Gamal Abd El Nasser, idadi ya misikiti elfu kumi ilijengwa, ambayo ni sawa na idadi ya misikiti iliyojengwa huko Misri kutoka kwa ushindi wa kiislamu hadi enzi ya Gamal Abd El Nasser.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, mada ya elimu ya dini ililazimishwa (somo la lazima) ikitegemea mafanikio au kutofaulu kama masomo mengine kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Misri, wakati ambapo ilikuwa hiari katika mfumo wa kifalme.
Katika enzi ya Abd El Nasser, Al-Azhar Al-Sharif iliundwa na kubadilishwa kuwa chuo kikuu cha kisasa ambapo sayansi za asili hufundishwa ndani yake pamoja na sayansi za kidini.
Bwana Mohamed Faeq katika kitabu chake cha (Abd El Nasser na Mapinduzi ya kiafrika) anasema kwamba Rais Abd El Nasser aliamuru ukuzaji wa Al-Azhar baada ya kufuata na kuangalia hali ya Waislamu barani Afrika, na alikuta kwamba nguvu za kikoloni za Magharibi zilikuwa na nia ya kuwafundisha Wakristo sayansi asilia (Utibabu - uhandisi – Dispensari ), na kutofundishwa kwa Waislamu, iliyosababisha utawala makundi ya Kikristo katika nchi za Kiafrika, ambao wengi wake ni Waislamu, na hawa Wakristo wachache walidhibiti nchi za kiafrika za kiislamu na walifanya kazi kama mfuasi anayedhamini masilahi ya nguvu za kikoloni za Magharibi zilizowafanya, kwa hivyo Rais Abd El Nasser alisisitiza kuvunja uhodhi huu wa madaraka na kuwafundisha waislamu waafrika sayansi tofauti za kisasa ili waweze kutawala nchi zao kwa faida ya nchi hizo.
Abd El Nasser alianzisha mji wa El Beooth wa Kiislamu , ambapo mamia ya maelfu ya wanafunzi waislamu walikuwa wakisoma na bado wakisoma katika eneo la ekari thelathini inayojumuisha wanafunzi wanaokuja kutoka nchi sabini za Kiislamu ili kujifunza huko Al-Azhar bure na kuishi nchini Misri kwa makazi kamili bure pia , na nchi ya Misri ilipewa maagizo kutoka kwa Rais Abd El Nasser kwa kuongeza mji huo kwa Uwezo wa kisasa na kuzidisha Idadi ya wanafunzi waislamu katika Al-Azhar kutoka nje ya Misri kuelekea mara kadhaa zaidi kwa sababu hii, Abd El Nasser aliunda Shirika la Mkutano wa Kiislamu uliojumuisha wananchi wote waaislamu, katika enzi ya Abd El Nasser, Qur'ani tukufu ilitafsiriwa kwa lugha zote za ulimwengu,katika enzi ya Abd El Nasser, Redio ya Qur'ani Tukufu iliundwa, ambayo hutangaza Qurani siku nzima.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, Qur'ani nzima ilirekodiwa kwenye rekodi kwa mara ya kwanza katika historia. Na Rais Abd El Nasser alikuwa mtawala mwislamu wa kwanza katika historia ya Uislamu anayekusanya Qur'ani Tukufu iliyosikika na kusomwa kwa sauti za wasomaji wakubwa wa Qur'ani Tukufu wakati wake. Na Rekodi na idhaa za Qurani tukufu zilienezwa Ulimwenguni kote.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, mashindano ya kusoma na kukariri Qurani yalipangwa katika ngazi ya Jamhuri, ulimwengu wa Kiarabu, na ulimwengu wa Kiisilamu, na Rais Abd El Nasser binafsi alikuwa akitoa tuzo za za wakariri wa Qurani.
Katika enzi ya Abd El Nasser, Maelezo ya Gamal Abd El Nasser kwa Fikihi ya Kiisilamu yalitolewa , ambayo ni pamoja na sayansi zote na Fikihi ya dini El Hanif , ziliwekwa katika idadi kubwa na kusambazwa ulimwenguni kote.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, maelfu ya taasisi za Al-Azhar na za kidini zilijengwa huko Misri, na matawi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar yalifunguliwa katika nchi nyingi za Kiislamu.
Gamal Abd El Nasser aliunga mkono nchi zote za Kiarabu na Kiislamu katika mapambano yake dhidi ya ukoloni.
Rais Gamal Abd El Nasser alikuwa mtawala wa Kiarabu na Mwislamu zaidi juu ya Uislamu na kueneza roho ya dini ya kweli katika haki ya kijamii na usawa kati ya watu.
Jumbe za kueneza Uislamu barani Afrika na Asia wakati wa Rais Gamal Abd El Nasser zilirekodi viwango vya juu zaidi vya kuingia katika dini ya Kiisilamu katika historia, wakati ambapo idadi ya wale waliochagua Uislamu kama dini kwa ufadhili wa misheni za Al-Azhar wakati wa Rais Gamal Abd El Nasser ilifikia watu 7 kutoka kati ya kundi la watu 10 na hivyo ni viasi visivyohakikishwa hapo awali katika historia kulingana na takwimu za Baraza la Makanisa la kidunia.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, sheria ilitolewa inakataza kamari na kuizuia, na Abd El Nasser alitoa uamuzi wa kufunga vilabu vyote vya Masoniki , Rotary na sherehe za Baha'i.
Wakati wa enzi ya Abd El Nasser, msichana kwa mara ya kwanza alifikia elimu ya dini, pia taasisi za Al Azhar zilifunguliwa kwa wasichana, na mashindano kadhaa yalifanyika katika miji yote kwa kusoma na kukariri Qur'ani Tukufu, mamilioni ya nakala za Qur'ani Tukufu zilichapishwa , zilipewa kwa nchi za Kiislamu na wajumbe walitumwa kutambua Uislamu barani Afrika na Asia pembe zote , Pia, vitabu vyote vya urithi wa Kiislamu vimechapishwa katika nyumba za kuchapisha za nchi , matoleo maarufu,ili vipatikane kwa wote.
Gamal Abd El Nasser alikuwa na hamu ya kufanya ibada za Ijumaa au kusali Ijumaa pamoja na na raia katika misikiti mikubwa wakati wa enzi yake.
Rais Gamal Abd El Nasser alikufa Jumatatu Septemba 28, 1970, ambayo inalingana na Hijri tarehe 27 Rajab 1390, roho safi ya Rais Gamal Abd El Nasser ilipanda kwa Muumbaji wake katika kumbukumbu ya siku ya Israi na Mi'raji, nayo ni siku ya sifa yake kuu ya kidini na hujulikana kwa wote.
Kuhusu dini ya Kikristo, uhusiano wa Rais Gamal Abd El Nasser ulikuwa bora na Papa Kyrillos VI, na Gamal Abd El Nasser aliyemwuliza Papa Kyrillos VI juu ya idadi ya makanisa ambayo anaona yanafaa kuyajenga kila mwaka, na majibu ya Papa yalikuwa (kutoka makanisa ishirini hadi thelathini), na Rais Abd El Nasser alikuwa aliyeamuru kwamba idadi ya makanisa yaliyojengwa kila mwaka iwe ishirini na tano, na idhini zake ziweze kuongozwa na Papa mwenyewe kwa taasisi rasmi.
Wakati Papa Kyrillos VI alimwomba Rais Abd El Nasser amsaidie kujenga jumba jipya linalofaa Misri, na kulalamikia kwakekwa ukosefu wa fedha za kutosha kulijenga kama alivyotamani, Rais Abd El Nasser mara moja akaamua kwamba nchi inachangia paundi 167,000 katika kujenga kanisa kuu mpya, na kwamba kampuni za ujenzi zinazohusika sekta ya umma zitatimiza kazi ya ujenzi wa kanisa mpya.
Pia , kulingana na maagizo ya Rais Gamal Abd El Nasser, mkutano wa kila wiki hufanyika kila Jumatatu kati ya Bwana Sami Sharaf - Waziri wa Mambo ya Urais wa Jamhuri - na Anba / Samweli - Askofu wa Huduma na Katibu wa Papa kwa ajili ya kujadili na kusuluhisha shida zozote zinazotokea kwa Wakiristo.
Rais Gamal Abd El Nasser pia alizingatia kukuza mahusiano ya karibu kati yake na Mtawala Hailaselasy, mtawala wa Habasha (Ethiopia), akichukua nafasi ya kuwepo kwa Wakristo wa Ethiopia ni kutoka jamii ya Orthodox. Na alimwita MtawalaHailaselasy ili kuhudhuria ufunguzi wa kanisa kuu mpya huko Abasya 1964, pia aliunga mkono wa kuunganisha makanisa mawili ya kimisri na kiethiopia chini ya uongozi wa Papa Kyrillos VI, Rais Abd El Nasser, kama ilivyo kawaida yake, mwenye jicho la siku za usoni , basi kwamba aliwahi kuwa kuunganisha viunganishi kati ya Misri na Ethiopia unahakikisha dhamana ya usalama wa kitaifa wa kimisri kwa sababu kilima cha Al Habasha inatoka kiasi cha 85% ya maji yanayofikia Misri kupitia mto wa Nili.
Kwa bahati mbaya, baada ya kifo cha Rais Abd El Nasser na mapambano dhidi ya mapinduzi mnamo Mei 13, 1971, na yaliyotokea baada ya vita vya Oktoba 1973 kwa sera za Abd El Nasser, mahusiano ya kimisri na Ethiopia yalizorota wakati wa Rais El Sadat, na bado zinaendelea kudhoofika hadi sasa, na Israeli ikachukua nafasi ya Misri nchini Ethiopia, na barani Afrika kote.
Katika enzi ya Gamal Abd El Nasser, hakukuwa na tukio moja la madhehebu kati ya Waislamu na Wakristo, na madai ya toba na uhasama wa mengine hayakuenea.
Gamal Abd El Nasser hakuwa adui kwa dini, wala hakuwa mtu anayekataa Mwenyezi Mungu kama wapinzani wake wa kisiasa kutoka kwa El Ekhwan El Moslmeen wamekuwa wakienea . bali, alikuwa mtawala mmisri wa karibu kwa uelewa wa roho ya dini na jukumu lake katika maisha ya watu na umuhimu wa kushirikiana katika haki na usawa ndani yake.