"Misri na Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote "
Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Harakati isiyofungamana upande wowote ilianzishwa na nchi zilizohudhuria Mkutano wa Bandung mnamo mwaka 1955 , na harakati hiyo ni matokeo ya vita kati ya pande hizo mbili (upande wa Ulaya , ukiongozwa na Marekani ambayo inajumuisha NATO) , ( na kambi ya mashariki, inayoongozwa na Umoja wa Kisovyeti, ambayo inajumuisha Warsaw Pact).

Misri inazingatiwa kuwa miongoni mwa nchi muhimu zaidi zilizoanzisha Harakati isiyofungamana kwa upande wowote, ambapo ina jukumu lake muhimu linalosifika kwa kuanzisha, kuunda na kuendeleza harakati hiyo, na katika kukuza kuwepo kwake na mwendelezo wake kutokana na umuhimu wake mkubwa wa kikanda na kimataifa kwa kuzingatiwa kuwa inajumuisha karibu na theluthi mbili ya nchi ulimwenguni zilizo wanachama katika Umoja wa Mataifa , vilevile inazingatiwa ni upande muhimu na mpana zaidi wa kuratibu misimamo ya nchi zinazoendelea kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayotolewa katika ajenda ya kimataifa. Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser anachukuliwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa harakati hiyo pamoja na Waziri Mkuu wa India Jawaharlal, Rais wa Yugoslavia Tito, na Rais wa Indonesia Ahmed Sukarno, na harakati hiyo inalenga kudumisha amani na usalama ulimwenguni na kukomesha Ukoloni kwa kiasi kikubwa , kutekeleza Uadilifu baina ya nchi ,kuheshimu kwa wanachama wote, kukuza maslahi ya pamoja, na kuheshimu haki za binadamu.
Misri ilikuwa na mchango wa wazi katika kubadilisha mawazo yanayohusiana na kutofungamana kwa upande wowote kuwa ukweli unaoonekana katika hali halisi wakati wa kuanzishwa kwa harakati hiyo . pia imekaribisha mkutano wa kilele wake wa pili mnamo mwaka 1964 , na mkutano wa 15 kwa viongozi na marais wa nchi ya harakati huko Sharm El. -Sheikh mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 11 hadi 16 Julai 2009. Mkutano huu unazingatiwa kuwa hatua wa kipekee katika mwendo wa harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa wa upande wowote katika karne ya ishirini na moja, kama ilivyokuwa mkutano wa Kairo mnamo mwaka 1964 ; wakati harakati ya ukombozi wa kitaifa ilikuwa kung'rika kwa hali ya juu ulimwenguni , mkutano huu wa kilele ulikuwa hatua wa kipekee katika historia ya harakati isiyofungamana na Upande Wowote, ambapo ulihamisha harakati hiyo kutoka kwa mfumo wa mfumo wa kisiasa hadi awamu ya maelezo ya kina , kushughulikiaji wa kina kwa maswala, na ilianzisha mchakato wa kupanga maswala kwenye ajenda kulingana na aina yake, jambo ambalo limekuwa la kuiga, au sehemu maalum katika taarifa zijazo za mwisho za harakati.

Utendaji ulio na kifani wa misri wakati wa uongozi wake kwa harakati ya isiyofungamana na Siasa wa upande wowote , ulichangia kufanikisha shughuli za harakati hiyo mnamo kipindi kilichopita, na kuwezesha harakati hiyo kuzungumza kwa sauti moja na kuitikia kadiri itakavyo kwa maendeleo yoyote yanayoweza kutokea katika uwanja wa kimataifa.
Misri ,tangu kushika kiti cha Uongozi wa mkutano wa 15 wa harakati ya kutofungamana na Siasa za upande wowote, imeendeleza mafanikio yaliyokufanywa na viongozi waliopita wa harakati hiyo ili kuimarisha nafasi yake katika ngazi ya kimataifa haswa katika mfumo wa Umoja wa Mataifa. vilevile , imeendelea kufanya juhudi na kuratibu na nchi zote wanachama ili kukamilisha kwa uaminifu utekelezaji wa Mpango wa Sharm El-Sheikh hadi Mkutano wa kilele ujao nchini Iran.
Nyaraka zilizotolewa na Mkutano wa Sharm El-Sheikh zilisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Kusini na Kusini kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine, kati yake na nchi zilizoendelea kiviwanda za Kaskazini , na kutahadharisha baadhi ya nchi za kiviwanda kuchukua maamuzi ya upande mmoja katika pande za uchumi, fedha na biashara ambazo zingeweza kuwa na athari mbaya mno kwa nchi zinazoendelea, pamoja na umuhimu wa Ushirikiano kati ya Kundi la 77 na harakati isiyofungamana na Siasa ya upande wowote , ambazo zinapishana katika malengo na Uchama; na Kundi la 15, ambalo lilitokana na harakati isiyofungamana na Siasa ya upande wowote katikati ya miaka ya 1980 mnamo karne ya ishirini na kwa kawaida hufanya mikutano yake pembeni mwa makongamano ya harakati hiyo .

Wakati wa uongozi wa Misri kwa harakati hiyo , imeshapitishwa uchama wa Azerbaijan na Visiwa vya Fiji pia kupitishwa kwa "tangazo la Bali" kwa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote kwa kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa harakati hiyo, ambalo limeainisha malengo na hatua za msingi za kukabiliana na machangamoto ya kisasa, na inaainisha maoni ya wanachama wa harakati hiyo juu ya masuala na machangamoto ya kimataifa wakati wa miaka ijayo.
Rais wa zamani Mohamed Morsi alishiriki katika Mkutano wa 16 wa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, ambao ulikaribishwa na mji mkuu wa Iran, Tehran, wakati wa kipindi cha kuanzia tarehe 30-31 Agosti 2012 , ambapo alihamisha uongozi wa mkutano huo kutoka Misri kuelekea Iran.
Ulimwengu na Mashariki ya Kati ulishuhudia matukio muhimu kati ya uongozi wa Misri kwa harakati katika mkutano wa kilele wa Sharm el-Sheikh mnamo 2009 , na mkutano wa kilele wa Iran mnamo Agosti 2021 , kuanzia na janga la kifedha ulimwenguni lililozuka katika Marekani na liliongezeka wakati wa urais wa Obama, kisha matukio ya mapinduzi ya kiarabu yakaendelea, kuanzia Tunisia na kupita Misri , Libya, Yemen na Syria, kujitenga kwa Sudan Kusini, kuondoka kwa majeshi ya Marekani kutoka Iraq, hata ikiwa imebaki chini ya udhabiti wa kijeshi na kisiasa wa Marekani. na imeongezeka udhibiti wa Iran ndani yake, na kuongezeka kwa vita vya kidiplomasia, vitisho, kuwekewa vikwazo na kususia Iran kwa sababu ya faili yake ya nyuklia na kuituhumu kwa kufanya kazi ili kutengeneza silaha za nyuklia. kutokana na hilo , umuhimu wa jukumu la harakati hiyo mbele ya maendeleo hayo muhimu limeonekana wazi katika uwanja wa kimataifa .
Mnamo Mei 4 , 2020, Rais Abdel Fattah El-Sisi alishiriki katika mkutano wa kilele wa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, ambao ulifanyika pamoja na anwani ya "Tuko pamoja katika Kukabilianana na Janga la virusi vya Corona", na hilo kwa kushirikisha marais kadhaa wa nchi na wanachama wa serikali ya harakati hiyo , inayoongozwa na Rais Ilham Aliyev, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan na Rais wa sasa wa Harakati hiyo, pamoja na Rais wa kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, na Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya. Mkutano huo umekuja kwa lengo la kujadili na kuratibu kati ya nchi wanachama katika harakati ya kutofungamana kwa upande wowote kuhusu athari za kuenea kwa janga la Corona, na kujadili njia za kukabiliana na janga hili katika nyanja zake zote za kiafya, kijamii na kiuchumi.
Rais El-sisi - Katika hotuba yake wakati wa mkutano huo - alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na mshikamano wa kimataifa kwa ajili ya jibu la maana na la haraka kwa janga la Corona, haswa kwa kufanya kazi ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa muhimu vya matibabu na kinga vinavyohitajika , kuongeza juhudi za utafiti wa kisayansi ili kuboresha dawa na chanjo ya virusi vya Corona, na juhudi za kimataifa za kusaidia nchi zinazoendelea na kutoa vifurushi vya kichocheo kwa uchumi wao, na kupunguza athari za janga hilo kwa usalama wa chakula Duniani.

vilevile ,Rais amesisitiza kuwa, harakati ya kutofungamana kwa upande wowote inapaswa kuchukua jukumu la msingi katika suala hili, na hilo wakati wa Misri ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha harakati hiyo, aidha kutokana na kwamba inazingatiwa ni mfumo muhimu na mpana wa kuratibu misimamo ya nchi zinazoendelea kuhusu masuala mbalimbali katika ajenda ya mfumo wa kimataifa.
Na mnamo Oktoba mwaka huo huo, pembeni mwa kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano wa mawaziri wa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote ulifanyika kwa ushiriki wa Waziri wa Mambo ya nje Sameh Shoukry kupitia mawasiliano ya kuona, ambapo Shoukry alisisitiza kipaumbele cha hali ya juu ambacho Misri inakiangalia katika harakati hiyo kwa kuwa ni mfumo muhimu ili kuratibu misimamo ya nchi zinazoendelea juu ya masuala mbalimbali yanatolewa katika ajenda ya mfumo wa kimataifa , Akiashiria umuhimu wa kushikamana kwa juhudi za wanachama wake kwa ajili ya kurejesha imani katika njia za kufanya kazi za pande nyingi na kukabiliana na mfumo wa siasa wa kuvutia katika mfumo wa kimataifa ili kuweza kukabiliana na changamoto nyingi zinazoukabili ulimwengu wetu hivi sasa .

Waziri Shoukry pia alisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja za harakati ili kupambana na ugaidi na kukomesha vyanzo vyake, kuanzisha eneo lisilo na silaha za maangamizi katika Mashariki ya Kati, na kutunga kanuni za kusimamia mtandao na kudumisha usalama wa Sebrania . Vile vile, amezungumzia msimamo thabiti wa Misri wa kuunga mkono kipaumbele cha masuluhisho ya kisiasa kwa mizozo ya Libya, Syria na Yemen, pamoja na haja ya kutafuta suluhisho la haki na la kina la suala muhimu la Palestina kwa mujibu wa maazimio ya uhalali wa kimataifa , jambo linalotekeleza matumaini halali ya watu wa Palestina ya kukomesha Ukoloni huo na kuanzisha nchi yao huru na mji mkuu wake ni Jerusalem Mashariki.
mnamo Juni 4, 2021, Balozi Dkt. Ahmed Ehab Gamal El-Din, mwakilishi wa kudumu wa Misri kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Geneva, alishiriki katika mkutano wa Mawaziri wa nchi za harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, unaofanyika pembezoni mwa kikao cha 109 cha Mkutano wa Kimataifa . Balozi Gamal El-Din - katika hotuba yake - alisisitiza kutilia maanani mwa Misri kwa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote kwa kuwa mmoja wa waanzilishi wake, akisisitiza jukumu lake muhimu katika mfumo wa pande nyingi na katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea ili kufikia mustakabali bora kwa watu wetu. aidha ,Balozi Gamal El-Din aligusia hatua zilizochukuliwa na Misri ili kupunguza athari za kiuchumi na kijamii za janga hili kwa kupitisha sera za fedha ili kuboresha uchumi Kutoa kiwango cha faida cha upendeleo kwa mikopo, kuchelewesha faida za kodi na mikopo, kuimarisha mfumo wa ulinzi ya kijamii, taratibu za ukaguzi wa wafanyikazi, utoaji wa posho kwa ajira wasiodumu, ambapo wanawake wanawakilisha 40%, kufadhili miradi ya wanawake, kuzindua programu za elimu ili kuwaunganisha katika soko la ajira, na kutoa huduma za mapumziko kwa wajawazito Na kutunza watoto na wanawake wenye ulemavu.
Mnamo Agosti 22, 2021, Balozi Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, alizungumzia Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, upanuzi wake, kujiunga na nchi zinazoendelea, na kufuatilia kanuni za nchi waanzilishi, akisema kwamba ilifika uwiano na utulivu katika mahusiano ya kigeni, wakati uliokuwa na mvutano, na kudhibitisha upande moja kwa upande mwingine,pia ilifanya kazi ili kufikia mahusiano ya usawa na kukidhi matarajio ya raia wanaoendelea kwa utulivu na maendeleo. Shoukry aliongeza, wakati wa hotuba yake katika mkutano na waandishi wa habari unaofanyika sasa hivi na mwenzake wa Serbia, Nikola Sekolavić, kwamba miaka iliyopita ilishuhudia mivutano na machangamoto mengi ambayo yaliathiri vibaya juu ya uwezo wa Harakati ya kutofungamana kutofikia malengo ambayo ilianzishwa kwa ajili yake . Shoukry aliomba kuwepo shughuli zaidi kati ya wanachama wa harakati hiyo, kuunda mipango kwa mustakabali, kuainisha machangamoto na kufikia hatua ya kuafikiana kuhusu jinsi ya kusonga mbele na harakati hiyo, kwa njia itakayotekeleza maslahi ya wanachama wake. Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesisitiza kuwa Misri inawajibika kuratibu, na inategemea mshikamano kati ya nchi za harakati hiyo na mashirika mengi ya kimataifa ili kuunda misimamo ya pamoja, na akiongeza kusema kwamba: "Wakati Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote inapozungumza kwa sauti moja, ni sauti yenye ushawishi na ufanisi ambayo inapitishwa."
Misri inaona kwamba Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote inazingatiwa mfumo muhimu na mpana zaidi wa kuratibu misimamo ya nchi zinazoendelea kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika ajenda ya Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono njia za kazi za pamoja za pande nyingi ili kukabiliana na sera za upande mmoja na za upande mmoja, ambazo ni mojawapo ya machangamoto makuu yanayokabilina nchi zinazoendelea, ambazo nyingi ni wanachama katika Harakati hiyo .
Misri inatilia maanani na harakati hiyo na haja ya kuihifadhi kutokana na umuhimu wake mkubwa wa kikanda na kimataifa, kwani inajumuisha karibu theluthi mbili ya nchi wanachama katika Umoja wa Mataifa ulimwenguni, kwa hiyo inazingatiwa kundi kubwa la upigaji kura, na inapaswa kufanya kazi ili kuimarisha mahusiano kati ya nchi zake ili kutetea maslahi yake na maslahi ya raia wake.
inazingatiwa Mojawapo ya mihimili mikuu inayoegemezwa juu yake msimamo wa Misri juu ya harakati ya kutofungamana na Siasa za Upande Wowote ambapo, harakati hiyo endapo ilianzishwa chini ya mfumo wa kimataifa wa pande mbili, basi tofauti ya mazingira hayo inalazimisha kuendeleza zana za harakati hiyo, jambo ambalo linaipa uwezekano wa kuchangia - kupitia misimamo chanya na ya kweli inayokubaliwa na nchi zake zote- Kuathiri mwendo wa mwingiliano wa kimataifa.
Misri inaamini kuwa, kile kinachoshuhudiwa katika uwanja wa kimataifa hivi karibuni katika suala la kuvunjwa kwa mihimili na misingi mikuu ambayo Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote iliegemezwa ni jambo la kutia wasiwasi haswa lile linalohusiana na kutoingilia katika masuala ya ndani ya nchi, kuheshimu hadhi yake , utulivu wake, na uhuru wa uamuzi wake, na kutotosheka kwa mamlaka ya kitaifa na umoja wa kikanda ili kuzuia Kuingilia mambo ya ndani ya nchi, badala yake, mambo ya ndani yenyewe yamekuwa kisingizio kwa wale wanaotaka kulazimisha udhibiti wao juu ya wengine, na haya yote ni machangamoto makubwa ambayo yanayowajibisha kuendelea kwa harakati pamoja na kuijenga upya na kukuza uwezo wake.
Nyaraka za harakati hiyo na mwendo wake zinathibitisha nafasi ya kihistoria iliyotekeleza - na Misri inatekeleza - katika kuendeleza harakati na kuingiza roho mpya katika mwili wake. na jukumu imara la kimisri imechangia katika kuanzisha na kuunda harakati ya kutofungamana na siasa za upande wowote pamoja na umuhimu wake wa ustaarabu na kisiasa ambao ni msingi unaozinatiwa na misri ili Kuunga m mwendo wa harakati hiyo katika siku zijazo kwa kuongeza juhudi zake za pamoja na nchi nyingi zinazofanya juu chini ili kuunga mkono harakati kwa lengo la kuendeleza malengo na mbinu zake, na kuifanya iwe na ufanisi zaidi kwa lile linalohusiana na kukabiliana na mabadiliko makubwa yanayotukia katika uwanja wa kimataifa kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni, hasa baada ya harakati hiyo ilibadilishwa kutoka chombo kinachojumuisha nchi 25 Katika mkutano wa kilele wake wa kwanza , kwa kuwa chombo kikubwa ambacho kwa sasa kinajumuisha nchi 118 za mabara ya Afrika, Asia, Ulaya, na Amerika ya Kusini.
Misri kwa ushiriki wake wa ufanisi katika mikutano ya Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote - tangu kuanzishwa kwa Harakati hiyo - inathibitisha mwingiliano wake wa endelevu na jukumu la uongozi lake, sio tu katika kanda yake lakini pia katika ngazi ya kimataifa katika kuonesha masuala ya nchi zinazoendelea ili ziweze kupata haki yake ya kisiasa na ya kimaendeleo katika nyanja ya kimataifa kutokana na imani yake kwa umuhimu wa kuimarisha kazi ya pamoja ya pande kadha kimataifa kupitia kuunga mkono wa Umoja wa Mataifa, mashirika na vyombo vyake, vinavyoongozwa na Baraza Kuu, kurekebisha na kuunda upya Baraza la Usalama la Umoja wa kimataifa kwa lengo la kulazimisha nchi wanachama kwa maamuzi yao, na sio kuzisukuma nchi hizi ili kufanya kazi nje ya mfumo wa kimataifa na mbali na mfumo wa uhalali wa kimataifa.