Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni Mzungumzaji katika Siku ya Wanawake wa Palastina

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ni Mzungumzaji katika Siku ya Wanawake wa Palastina

Machi 26, 2022, kama kumbukumbu ya Siku ya Wanawake wa Palastina, Magada Hashem, Mwanachama wa Harakati ya Vijana ya Nasser, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, pia Mwanachuoni wa Kitivo cha Sanaa za Ufundi, Chuo kikuu cha Al-Najah ya kitaifa ,Palastina, akiwakilisha  Harakati ya Vijana ya Nasser huko Palastina, alishiriki katika mpango wa "Asira Btasalem Alek" kama mjumbe wa kamati ya maandalizi katika Mpango huo, pamoja na Ushirikiano wa: Mtaa wa Asira wa Kaskazini, Jumuiya ya Zaat Al-Nataqatin Al-Asiri, na Taasisi ya CARE ya Kimataifa, inayolenga kuwekeza Rasiliamali za Palastina huko Asira ya Kaskazini, kama Rasiliamali Asili, Watu, zinazohusu mahali na wakati pia, na kuziendeleza Kiutamaduni, kiutalii na kiuchumi. 

Katika muktadha huo, Ushiriki wa Harakati ya Vijana ya Nasser ulipatikana kwa nakshi kauri kikubwa na  “Hamiyat al-Dar”, iliyochongwa na “Magada Hashem”, pamoja na brashi yake ya kisanaa yenye matumaini, pamoja na mtazamo wa kiarabu, na maoni ya Nasser kwa kuimarisha ufahamu na nguvu za kienyeji huko Palastina, na ambamo mtazamo kwa mwanamke mwarabu wa Kipalestina inaonekana wazi, Mlinzi wa Nyumba , Moto na Mlinzi wa Nyumba ya kiarabu.Nazo ni sehemu ndogo ya  kisanaa ili kuhusisha sanaa katika mchakato wa Mwamko wa Palastina, Uthabiti pia Changamoto.

Kwa upande wake, Mchoraji , Magada Hashem, alielezea ushiriki wake katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akisema, "Uzoefu huo ulinipa msukumo wa kiutamaduni wa kiarabu na kibinafsi, ambao niliionesha katika kazi zangu za sanaa na Ushiriki wangu wa jamii huko Palastina.

 Pia nilinuia kuwa na mchango wa kwanza katika kuanzisha, Kujitolea,na kuongoza ndani ya jamii, nikifuatilia marafiki wa Nasser wenye ushawishi katika jamii zao za nchi za Duniani kote, basi Udhamini wa Nasser hukupa jukumu kubwa la kubadilisha na kushawishi katika nchi yako."

 

Alihitimisha maneno yake akionesha kuwa Jaribio lake la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa lilimpa moyo ya kusonga mbele na 

 kuhamisha jamii, Sura, Utambulisho, Utu na mambo ya Palastina kwa watu wa Dunia, kama lilivyofanya na wahitimu wote wa Udhamini huo,basi liliwafanya wawe na hamu ya kufikisha sauti ya nchi zao pamoja na Utambulisho wa asili kwa Utu mzima.