Mwanachama wa kufundisha wa Udhamini wa Nasser .., ni Waziri Mwakilishi kwenye Sekta ya kidiplomasia ya kimisri

Mwanachama wa kufundisha wa Udhamini wa Nasser  .., ni Waziri Mwakilishi kwenye Sekta ya kidiplomasia ya kimisri
Mwanachama wa kufundisha wa Udhamini wa Nasser  .., ni Waziri Mwakilishi kwenye Sekta ya kidiplomasia ya kimisri
Mnamo Alhamisi 16 Julai 2020, Rais Abd El Fatah El-Sisi ameidhinisha harakati za kukuza idadi ya washiriki wa Sekta ya kidiplomasia kwenye Wizara ya Mambo ya nje ya kimisri, na Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ulikuwa pamoja na kumheshimu Dokta Marwa Salem kutoka kwa nafasi ya " Mshauri" akiwa" Waziri Mwakilishi" , na hivyo ni miiongoni mwa wanachama 211 waliopata kuinua katika Sekta ya kidiplomasia, mabalozi 7 ambao walipandishwa kwa mabalozi wa kitengo bora, mawaziri 20 waliokabidhiwa na wawe mabalozi, washauri 35 wawe katika nafasi ya mawaziri wakilishi, makatibu wa awamu ya kwanza 38 wawe katika kiwango cha mshauri, makatibu wa awamu ya pili 42 kwa Nafasi ya katibu wa awamu ya kwanza, na makatibu wa awamu ya tatu 43 wawe katika kiwango cha katibu wa awamu ya pili , Na Maafisa 26 wawe katika kiwango cha katibu wa awamu ya tatu.
Dokta Marwa Mamdouh ni Mwanadiplomasia, Mwanachuoni, na Mtafiti wa mahusiano ya kimataifa. Ameshapata digrii ya shahada ya kwanza katika Uchumi na Sayansi za kisiasa , Chuo Kikuu cha Kairo mnamo 1997, kisha akapata diploma ya juu katika masomo ya Afro-Asia kutoka Chuo Kikuu cha Khartoum, Chuo cha Masomo ya Kiafrika na Asia mnamo 2006, Cheti ya Uzamili katika masuala ya Kiafrika, Chuo Kikuu cha London, Kitivo cha Masomo ya Mashariki na kiafrika, juu ya malengo na matokeo ya sera ya Israil ya Kiafrika mnamo 2009, na pia akapata digrii ya Uzamili katika masuala ya Ulaya Mashariki na Urusi kutoka Chuo Kikuu Huru cha Berlin 2020, na akapata dirigii ya Uzamivu katika falsafa kutoka Chuo Kikuu cha London, Kitivo cha Masomo ya Mashariki na Afrika, kuhusu changamoto zinazoikabili sera ya Misri ya Kiafrika (Utafiti wa shida ya maji ya Nile na Uanachama wa Misri katika Umoja wa Afrika) mnamo 2016.
pamoja na kuwepo kwake hatua kwa hatua katika safu za Wizara ya Mambo ya nje ya kimisri tangu mwaka 1999 hadi sasa kutoka kwa Afisa hadi awe Waziri Mwakilishi, amekuwa akifanya kazi katika uwanja wa utafiti wa kisiasa na kazi ya masomo, kwa vile alifanya kazi katika uwanja wa utafiti wa kisiasa na shughuli za mafunzo, basi amefanya kazi kama mtafiti wa kisiasa katika mahusiano ya kimataifa katika Kituo cha Al-Ahram cha Mafunzo ya Kisiasa na kimikakati, na pia alifanya kazi kama Mwanachuoni katika uwanja wa mahusiano ya Kimataifa , akizingatia mambo ya Kiafrika kwa upande mmoja, na masuala ya Urusi na Mashariki ya Ulaya kutoka upande mwingine. Dokta Marwa amefundisha katika miji mikuu kadhaa ya Kiafrika na Ulaya, pamoja na Khartoum, Djibouti, Kigali, Adis Ababa, London, Helsinki na Berlin. Yeye pia amefundisha katika vyuo vikuu vingi vya kimisri, na ana makala nyingi na nakala za utafiti zilizochapishwa huko Misri, Urusi na Ujerumani, pamoja na ushiriki wake katika mikutano na semina nyingi za kimataifa kwa lugha za kiarabu, kiingereza na kifaransa.
Inatajwa kwamba Dokta Marwa Mamdouh, Mwanachama wa timu ya kufundishia katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, ikiambatisha picha za mhadhara wa mwisho wakati wa ziara ya washiriki wa Udhamini kwa Makumbusho ya kiongozi Gamal Abd El Nasser , kuhusu Makumbusho ya kiongozi marehemu Gamal Abd El Nasser, amezungumzia mhusika wa Gamal Abd El Nasser , maisha yake, ukuaji wake, sifa zake za kipekee barani Afrika , pamoja na mchango wake wa kukuza nchi na jukumu lake katika kusaidia na kuunga mkono harakati za ukombozi barani Afrika.