Gamal Abdel Nasser na kupoteza Sudan

Gamal Abdel Nasser na  kupoteza  Sudan

Na / Amr Sabeh

Imefasiriwa na / Nour Khaled

kabla ya kuzaliwa Gamal Abdel Nasser kwa miaka 19, Sudan imetengana na Misri, na kuwekwa mipaka kati ya nchi hizo mbili kumefanyikwa kabla ya kuzaliwa kwake kwa miaka 12, na hata Katiba ya 1923  ambayo imetoa uamuzi kupata lakabu ya Mahakama za Misri kwa lakabu ya Mfalme mmisri na kuondosha lakabu ya Sudan imefanyikwa wakati  Gamal Abdel Nasser alikuwa na umri wa miaka 5, Alipokuwa na umri wa miaka sita, Misri ilijitenga na Sudan kijeshi, na wakati Misri na Sudan zimetenganishwa na eneo la maji, Mheshimiwa Gamal Abdel Nasser alikuwa na umri wa miaka 11, wakati huu Mheshimiwa Waziri Mkuu Mostafa Al-Nahas amekubali kupata haki za Kujiamulia kwa Sudan mnamo 1937, wakati Mheshimiwa Gamal Abdel Nasser alikuwa na umri wa miaka 19, na amejiunga Kitivo cha Kijeshi mwaka ule ule.

Mtawala wa mwisho miongoni mwa familia ya Mohamed Ali aliyeruhusiwa na ukoloni wa Kiingereza kupiga ziara kwa Sudan, Khedive Abbas Helmi 2 aliyepiga ziara kwa Sudan mnamo 1902, na baadaye watu kutoka familia ya Mohamed Ali hawakufikia Sudan tena, hadi tukio la Kubomoa kwa Mfalme Farouk na kufukuzwa kwake kutoka Misri mnamo Julai 26,1952.


Wakati wa utawala wa familia ya Muhammad Ali Pasha, hakuna kitengo chochote cha serikali huko nchini  Misri kinachojumuisha Waziri kutoka Sudan, sawa na vile vile hakuna msudan yeyote  alichaguliwa katika mabunge ya Misri tangu kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi mnamo mwaka wa  1866 wakati wa utawala wa Khedive Ismail hadi bunge la mwisho pamoja na Seneti wakati wa utawala wa Mfalme Farouk wa kwanza.

Na hata hakuna sarufu yoyote ya kifedha nchini Misri wakati huu ina maandishi ya majina mawili  ya mfalme wa Misri na wa  Sudan. Lakini sarufu zozote zina maandishi ya jina la mfalme wa Misri tu.

Na hata baraza la mabunge imekubalika kutengana Misri na Sudan mnamo mwaka wa 1951, kabla ya mapinduzi ya Gamal Abdel Nasser kwa mwaka mmoja. 

Na wakati Mostafa Al-Nahas alipofuta makubaliano mwaka wa 1936 mnamo  Oktoba 8, 1951, na ametoa makubaliano ya Utawala wa pamoja kwa Sudan, wakati huu serikali yake imetoa ajenda ya mswada kuwa Sudan imekuwa na Katiba ya binafsi imewekwa na jumuiya inajumuisha wasudan, na hayo yote inamaanisha Utambuzi wa uhuru wa Sudan kutoka Misri.

Ni maana gani kwa hali ya Sudan iwe na  Katiba mpya kupitia watu wake nayo iko tofauti na Katiba ya Misri!?


Gamal Abdel Nasser amejaribu kwa njia zote kuungana Misri na Sudan kwa ajili ya raia wa Bonde la Nile tangu siku ya kwanza ya mapinduzi.  Lakini  Waingereza wamepanga kutengana kati ya Misri na Sudan tangu wakati wa awali ili kuwakalia kumiliki  kwa Misri mnamo 1882, kabla ya Gamal Abdel Nasser amezaliwa hata kwa miaka 36, na kweli wamefanikiwa kufanya hicho kupita maafisa wanasiasa kutoka Sudan, na haswa hayati Ismaili Al-Azhari anayebadilika msimamo wake kutoka anayehamisisha kuungana kati ya Misri na Sudan kwa kiongozi wa kutengana Sudan na Misri.  

Na wakati Gamal Abdel Nasser alipotambua kuwa maafisa wa Sudan wametaka kuongoza Sudan,  mbali na kuungana na Misri,  na kwa hivyo amekubali kutaka kujiamulia na kwa kitendo ameweza kufikia kutengana Sudan na Misri.


Vyanzo:

Katika Baada ya Mapinduzi ya Misri.. Sehemu ya Kwanza na Sehemu ya Pili: Abd al-Rahman al-Rafi'i .

Mustafa Kamel, Mwanzilishi wa vuguvugu la kitaifa: Abd al-Rahman al-Rafi'i.

 Misri na Sudan: Kutengana kwa Nyaraka za Siri: Mohsen Mohamed. 

Abdel Nasser na Mapinduzi ya Afrika: Mohamed Fayek.