Baraza la Udhibiti wa Mapinduzi
Baraza la Udhibiti wa Mapinduzi liliundwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Julai 23,1952.
Na Jenerali Mohammed Nagib alishika uongozi wa Baraza hilo kuanzia mwaka 1952 hadi mwaka 1954, na mnamo mwaka wa 1953, agizo la kijamhuri lenye Na. 1 lilitolewa kwa kumteua Meja Mohammed Abdulhakim Amer awe Kiongozi mkuu wa Jeshi na alimpa nafasi ya Jenerali. Kisha Baraza la Udhibiti wa Mapinduzi liliongozwa na Al-Bakbashi Gamal Abdel Nasser kuanzia mwaka wa 1954 hadi mwaka wa 1956.
Baraza la Udhibiti wa Mapinduzi liliongoza Utawala wa Misri kuanzia Novemba 14, 1954 hadi Juni 24,1956.